Kusanidi IR Blaster ili kudhibiti set-top box (kisanduku cha kebo/satelaiti) (Modeli zinazotangamana na modeli za IR Blaster pekee)
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mipangilio.
Kutekeleza [Usanidi wa udhibiti wa set-top] katika [Usanidi wa IR Blaster] hukuwezesha kutumia kisanduku cha kebo/satelaiti kutoka kwenye menyu iliyoonyeshwa kwa kubonyeza kitufe cha ACTION MENU kwenye rimoti.
- Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Ingizo za nje] — [Usanidi wa IR Blaster] — [Usanidi wa udhibiti wa set-top].
- Fuata maagizo kwenye skrini.
Kidokezo
Kumbuka
- Baadhi ya vifaa vya nje huenda visiitikie baadhi ya vipengee katika “Menyu ya Kitendo”.
- Ukibonyeza na ushikilie kitufe kwenye rimoti, huenda shughuli isifanye kazi. Badala yake, jaribu kubonyeza kitufe kwa kurudia.