Kucheza maudhui kutoka kwenye kompyuta
Unaweza kufurahia maudhui (faili za picha/muziki/video) yaliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mtandao kilicho katika chumba kingine, ukiunganisha TV kwa mtandao wa nyumbani kupitia kipanga njia.
- Kompyuta (seva)
- Kipanga njia
- Modemu
- Intaneti
- Unganisha TV kwenye mtandao wako wa nyumbani.
- Bonyeza kitufe cha HOME, chagua (ikoni ya Programu) kutoka kwenye Menyu ya mwanzo, na uchague [Albamu], [Video], au [Muziki] kutoka kwenye orodha ya programu.
Ikiwa rimoti iliyokuja nayo ina kitufe cha APPS, unaweza kubonyeza kitufe cha APPS ili kuonyesha orodha ya programu. - Bonyeza kitufe cha (Kushoto) na uteue jina la seva kwenye menyu iliyoonyeshwa.
- Chagua folda au faili ili kucheza kutoka kwenye orodha.
Ukichagua folda, chagua faili unayotaka.
Uchezaji huanza.
Kukagua fomati za faili zinazokubaliwa
Kumbuka
- Kulingana na faili, uchezaji huenda usiwezekane hata wakati wa kutumia fomati zinazokubaliwa.