Chapisha

Menyu ya nyumbani

Skrini iliyoonyeshwa wakati unapobonyeza kitufe cha HOME kwenye rimoti huitwa Menyu ya Mwanzo. Kutoka kwenye Menyu ya Mwanzo, unaweza kutafuta maudhui na kuchagua maudhui, programu, na mipangilio inayopendekezwa.

Kielelezo cha skrini ya Menyu ya nyumbani kinaonyeshwa kwenye skrini ya TV

Utafutaji, Taarifa, Ingizo, Kipima saa, na Mipangilio (A)

Maikrofoni / Kibodi ya kwenye skrini:
Tumia maikrofoni kwenye rimoti au kibodi kwenye skrini iliyoonyeshwa kwenye TV ili kuingiza maneno msingi na kutafuta maudhui mbalimbali. Kwa utafutaji wa sauti, rejelea ukurasa wa Kutumia maikrofoni inayodhibitiwa na rimoti.
(Arifa):
Huonyeshwa wakati kuna arifa kama vile kukiwa na tatizo la muunganisho au sasisho la programu. Nambari huashiria idadi ya taarifa.
(Ingizo):
Hubadilisha kifaa ingizo kilichounganishwa kwenye TV.
(Kipima saa):
Sanidi [Kilalishaji cha Majira].
Kwa maelezo, rejelea ukurasa wa [Kipima saa].
(Mipangilio):
Sanidi mipangilio kadhaa inayohusiana na TV. Kwa maelezo, rejelea ukurasa wa [Mipangilio].

Programu (B)

Onyesha programu zako uzipendazo.

  • Ukichagua [Programu], orodha ya programu zilizosakinishwa huonyeshwa.
  • Chagua [Ongeza programu kwenye vipendwa] ili kuongeza programu kwenye vipendwa.
  • Ukichagua programu iliyoongezwa na ubonyeze na ushikilie Ingiza kitufe katika rimoti, unaweza kubadilisha mpangilio au kuondoa kipendwa.

Zinazofuata (C)

Huonyesha unachoweza kutazama baadaye kulingana na maudhui.

Kumbuka

  • Ikiwa hakuna maudhui yanayotumika, huenda [Zinazofuata] isionyeshwe.

Vituo (D)

Safumlalo zilizo chini ya Programu (B) / Zinazofuata (C) zinaitwa “Vituo”. Hapa, unaweza kutazama maudhui kutoka kwenye huduma za upeperushaji, au utiririshaji wa video.

Kidokezo

  • Historia ya hivi karibuni ya vituo huonyeshwa kwenye [Runinga].
  • Unaweza kuongeza maudhui kwenye Zinazofuata kwa kuchagua maudhui kwenye kituo chochote na kubonyeza na kushikilia kitufe cha Ingiza katika rimoti.
  • Katika Menyu ya Nyumbani, unaweza kupanga safu wima kutoka kwa “Vituo (D)” na chini. Tumia vitufe vya juu / cihni kusogeza angalizo kwenye ikoni ya mviringo katika safumlalo unayotaka kusogeza, na ubonyeze kushoto (au kulia kulingana na lugha ya uonyesho ya TV) ili uweze kusogeza safumlalo juu au chini kwa kubonyeza vitufe vya juu / cihni.

Badilisha vituo utakavyo (E)

[Badilisha vituo utakavyo] hutumika kuonyesha au kuficha vituo vilivyochaguliwa.