Chapisha

Kutumia Mwongozo wa Usaidizi

Mwongozo Huu wa Usaidizi unafafanua jinsi ya kutumia TV hii. Unaweza pia kurejelea Setup Guide kwa maelezo kuhusu kusakinisha TV, na Reference Guide kwa maelezo ya vipande, ainisho, na kuweka TV hii kwenye ukuta.

Katika Mwongozo huu wa Usaidizi, unaweza kusoma taarifa unayotaka au kuitafuta moja kwa moja. Ili utafute, teua ikoni ya utafutaji juu ya skrini.

Kumbuka

  • Ili utumie vipengele vipya vilivyofafanuliwa katika Mwongozo wa Usaidizi, huenda ukahitaji kusasisha programu ya TV. Kwa maelezo kuhusu visasisho vya programu, angalia ukurasa wa Sasisho za programu.
  • Majina ya mipangilio katika Mwongozo wa Msaada yanaweza kutofautiana na yale yanayoonyeshwa kwenye TV kulingana na tarehe ya toleo la TV au modeli/nchi/eneo lako.
  • Picha na vielelezo vinavyotumiwa katika Mwongozo wa Usaidizi huenda vikawa tofauti kulingana na modeli ya TV yako.
  • Muundo na ainisho zinaweza kubadilika bila notisi.

Kidokezo

  • Ili kuona kama TV yako ina moja ya vitendaji vilivyoelezewa katika Mwongozo wa Usaidizi, rejelea mwongozo wa karatasi au katalogi ya bidhaa ya Sony.
  • Mwongozo huu wa Usaidizi umeandikiwa maeneo/nchi zote. Baadhi ya maelezo yaliyo katika Mwongozo huu wa Usaidizi hayatumiki kwa maeneo na nchi nyingine.