Chapisha

Temino ya kuunganisha

Aina na maumbo ya viunganishi hutofautiana kulingana na TV yako.
Kwa eneo la viunganishi, rejelea Setup Guide (mwongozo uliochapishwa).

Temino Maelezo
Picha ya kituo cha USB
USB
Huunganisha kwenye Kamera ya dijitali ya picha/Kamkoda/midia ya hifadhi ya USB.

Kumbuka

  • Kuunganisha kifaa kikubwa cha USB kunaweza kuingiliana na vifaa vingine vilivyounganishwa kando yake. Katika hali hizo, unganisha kwenye kituo kingine cha USB.
Picha ya jeki ya AV IN
AV IN
Huunganisha kwenye VCR/vifaa vya mchezo wa Video/Kichezaji cha DVD/Kamkoda.
Kwa muunganisho sawia, rejelea Kuunganisha Blu-ray au kichezaji cha DVD.
Picha ya jeki ya Kifaa cha kichwa
(Kifaa cha kichwa)
Huunganisha kwenye jeki ya kifaa cha kichwa ili kusikiliza sauti kutoka kwenye TV. Hukubali jeki ndogo ya stereo yenye sehemu tatu pekee.

Kumbuka

  • Huwezi kutoa sauti kutoka kwenye kifaa cha masikio na spika za TV kwa wakati mmoja.
Picha ya temino ya HDMI IN
HDMI IN
Huunganisha kwenye kifaa cha HDMI. Kiolesura cha HDMI kinaweza kuhamisha video ya dijitali na sauti kwenye kebo moja. Ili kufurahia maudhui ya hali ya juu ya 4K, unganisha Premium High Speed HDMI Cable(s) na uweke [Umbizo la wimbi la HDMI] kwa [Umbizo lililoboreshwa].
Picha ya temino ya HDMI IN ARC
HDMI IN ARC (Kituo cha Kurejesha Sauti)
Huunganisha mfumo wako wa sauti kwenye HDMI IN ARC ili kuelekeza sauti ya TV kwenye mfumo wako wa sauti. Ni kipengele ambacho hutuma sauti kwenye mfumo wa sauti ambao unakubali ARC kupitia kebo ya HDMI. Ikiwa mfumo wa sauti haukubali ARC, unahitaji kuunganisha na DIGITAL AUDIO OUT (OPTICAL).
Picha ya jeki ya DIGITAL AUDIO OUT (OPTICAL)
DIGITAL AUDIO OUT (OPTICAL)
Huunganisha mfumo wa sauti na ingizo la sauti optiki.
Unapoungnaisha mfumo wa sauti usiotangamana na ARC kwa kutumia kebo ya HDMI, unahitaji kuunganisha kebo ya sauti ya optiki kwenye DIGITAL AUDIO OUT (OPTICAL) ili utoe sauti ya dijitali.
Picha ya temoni ya ANTENNA
(Ingizo la Kebo/Antena)
Huunganisha kwenye Kebo/Antena/Kisanduku cha Nje.
Picha ya kituo cha LAN
LAN
Huunganisha kwenye Kipanga njia.
Huunganisha kwenye Intaneti kwa kutumia kebo ya LAN.