Kurekebisha mfumo wa sauti
Baada ya kuunganisha mfumo wa sauti kwenye TV, rekebisha sauti towe ya TV kutoka kwenye mfumo wa sauti.
Kurekebisha mfumo wa sauti uliounganishwa na kebo ya HDMI au kebo optiki ya dijitali
- Baada ya kuunganisha TV kwenye mfumo wako wa sauti, bonyeza kitufe cha HOME, na uchague yafuatayo kwa utaratibu.
- Washa mfumo wa sauti uliounganishwa, kisha rekebisha sauti.
Ukiunganisha kifaa kinachoingiana na CEC ukitumia muunganisho wa HDMI, unaweza kukiendesha kwa kutumia rimoti ya TV tu.
Kumbuka
- Unahitaji kusanidi mipangilio ya [Zao la sauti dijito] kulingana na mfumo wako wa sauti. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Zao la sauti dijito].
- Kama mfumo wa sauti hautangamani na Dolby Digital au DTS, weka [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Zao la sauti dijito] kwenye [PCM].