Chapisha

Kutumia vipengele vinavyopatikana kwa vifaa vinavyotangamana na CEC

Kichezaji cha Blu-ray/DVD

  • Huwasha kichezaji Blu-ray/DVD na kubadilisha ingizo kuwa kichezaji Blu-ray/DVD unapokiteua kutoka kwenye chanzo cha ingizo.
  • Huwasha TV moja kwa moja na hubadilisha ingizo la kichezaji kilichounganishwa cha Blu-ray/DVD wakati kichezaji cha Blu-ray/DVD kinapoanza kucheza.
  • Huzima kichezaji kilichounganishwa cha Blu-ray/DVD wakati unapozima TV.
  • Hudhibiti shughuli za menyu (vitufe juu / cihni / kushoto / kulia), uchezaji (n.k., vitufe vya Cheza), na uchaguaji idhaa kwa kichezaji kilichounganishwa cha Blu-ray/DVD kupitia rimoti ya TV.

Kipokea AV

  • Huwasha kiotomatiki kipokea AV kilichounganishwa na huwasha sauti towe kutoka kwa spika ya TV hadi mfumo wa sauti wakati unapowasha TV. Kitendaji hiki kinapatikana tu ikiwa umetumia awali kipokea AV kwa sauti towe ya TV.
  • Hubadilisha kiotomatiki sauti towe ya kipokea AV kwa kuwasha kipokea AV wakati TV imewashwa.
  • Huzima kipokea AV kilichounganishwa kiotomatiki wakati unapozima TV.
  • Hurekebisha vitufe vya sauti (vitufe vya Sauti +/−) na hunyamazisha kitufe cha sauti (kitufe cha Nyamazisha) cha kipokea AV kilichounganishwa kupitia rimoti ya TV.

Kamera ya video

  • Huwasha TV moja kwa moja na hubadilisha ingizo la kamera ya video iliyounganishwa wakati kamera imewashwa.
  • Huzima kamera ya video iliyounganishwa kiotomatiki wakati unapozima TV.
  • Hudhibiti operesheni ya menyu (vitufe juu / cihni / kushoto / kulia), uchezaji (n.k., vitufe vya Cheza), wa kamera ya video iliyounganishwa kupitia rimoti ya TV.

Kumbuka

  • CEC” inapatikana tu kwa vifaa vilivyounganishwa vinavyooana na CEC.
  • Tabia ya vifaa vya CEC inaweza kutofautiana.