Kurekebisha mipangilio ya HDMI CEC
- Washa kifaa kilichounganishwa.
- Ili kuwezesha [HDMI CEC Mipangilio], bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Ingizo za nje] — [HDMI CEC Mipangilio] — [CEC].
- Wezesha HDMI CEC Mipangilio kwenye kifaa kilichounganishwa.
Chaguo zinazopatikana
Chaguo zinazopatikana huonyeshwa hapa chini. (Chaguo hutofautiana kulingana na modeli/eneo/nchi yako.)
- [Uzimaji oto wa vifaa]
- Ikilemazwa, kifaa kilichounganishwa hakizimwi kiotomatiki wakati TV imezimwa.
- [Uwashaji oto wa Runinga]
- Ikilemazwa, TV haiwaki kiotomatiki wakati kifaa kilichounganishwa kimewashwa.