Chapisha

Kusakinisha programu kutoka kwenye Google Play Store

Unaweza kupakua programu kutoka Google Play Store na kusakinisha kwenye TV, kama unavyofanya katka simu maizi na kompyuta kibao.

Kumbuka

  • Unaweza tu kusakinisha programu ambazo zinaoana na TV. Huenda zikatofautiana na programu za simu maizi/kompyuta kibao.
  • Muunganisho wa Intaneti na akaunti ya Google zinahitajika ili kupakua programu kwenye Google Play Store.

Kidokezo

  • Ikiwa huna akaunti ya Google au unataka kuunda akaunti iliyoshirikiwa, unda akaunti mpya kwa kufikia tovuti ifuatayo.
    https://accounts.google.com/signup https://accounts.google.com/signup
    Tovuti hapa juu inaweza kutofautiana kulingana na eneo/nchi yako. Pia inaweza kubadilika bila ilani. Kwa maelezo, rejelea ukurasa wa mwanzo wa Google.
  • Tunapendekeza kwamba uunde akaunti ya Google kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi.
  1. Bonyeza kitufe cha HOME, chagua (ikoni ya Programu) kutoka kwenye Menyu ya mwanzo, na uchague Google Play Store kwenye orodha ya programu.
    Ikiwa rimoti iliyokuja nayo ina kitufe cha APPS, unaweza kubonyeza kitufe cha APPS ili kuonyesha orodha ya programu.
  2. Chagua programu ya kusakinisha.

Baada ya kupakua, programu inasakinishwa na kuongezwa kiotomatiki. Aikoni yake hutokea kwenye orodha ya programu zilizosakinishwa, hivyo kukuruhusu kuianzisha.

Kuhusu programu- zinazolipiwa

Kuna programu za bila malipo na programu zinazolipiwa katika Google Play Store. Ili kununua programu inayolipiwa, msimbo wa kadi ya zawadi iliyolipiwa awali ya Google Play au taarifa ya kadi ya mkopo inahitajika. Unaweza kununua kadi ya zawadi ya Google Play kutoka kwa wauzaji rejareja mbalimbali.

Ili kufuta programu

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, chagua (ikoni ya Programu) kwenye Menyu ya mwanzo, chagua Google Play Store kwenye orodha ya programu, na uchague Programu Zangu.
    Ikiwa rimoti iliyokuja nayo ina kitufe cha APPS, unaweza kubonyeza kitufe cha APPS ili kuonyesha orodha ya programu.
  2. Chagua programu ya kufuta, na kisha uisakinushe programu hiyo.