Chapisha

Kuonyesha skrini ya simu maizi/kompyuta kibao kwenye TV kwa kutumia Utendaji wa Kuakisi skrini

Unaweza kuonyesha skrini ya kifaa cha mkononi kwenye TV ili kuona picha, video au tovuti.

Kipengele cha “Uakisi wa skrini” hutumia teknolojia ya Miracast kuonyesha skrini ya kifaa kinachotangama kwenye TV. Kipanga njia pasiwaya sio lazima kitumike kwa kitendaji hiki.

Illustration of content sharing
  1. Simumahiri
  2. Kompyuta kibao
  3. Kompyuta
  1. Bonyeza kitufe cha (Weka uteuzi), kisha uteue [Uakisi wa skrini].
  2. Tumia kifaa chako kinachotangamana na Uakisi wa skrini ili uunganishe kwenye TV.
    Wakati kifaa kimeunganishwa kwenye TV, skrini inayoonyeshwa kwenye kifaa itaonyeshwa pia kwenye TV.
    Kwa maelezo, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa chako.

Kumbuka

  • Wakati skrini ya kusubiri ya Uakisi wa skrini imeonyeshwa, muunganisho pasiwaya kati ya runinga na kipanga njia chako pasiwaya utatenganishwa, kwa hivyo mawasiliano kupitia Intaneti hukomeshwa.